Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 18, 2014

ASKARI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUIBA MTOTO WA UMRI WA SIKU SABA

ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto  
Baba Mzazi  wa mtoto aliyeibiwa  Salehe Issah Mwangosi(31) ndiye alieshirikiana na polisi huyo kumwiba mtoto

 Mboka Mwakikagile(20) mama mzazi wa mtoto aliyeibiwa



ASKARI wa Jeshi la Polisi aliyefahamika kwa jina la Prisca Kilwai mwenye namba WP 5367 wa Ilala Jijini Dar es Salaam amekamatwa kwa tuhuma za wizi wa mtoto jinsi ya kiume aliyefahamika kwa jina la Goodluck Salehe(siku 7) aliyeibwa April 6 mwaka huu huko Kasumulu Kata ya Itope Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Mtoto alizaliwa Machi 30 na alipoibiwa alikuwa na umri wa siku sita ambapo mtuhumiwa alishirikiana na Baba Mzazi aliyefahamika kwa jina la Salehe Issah Mwangosi(31) mkazi wa Matankini Kyela aliyemtambulisha kwa mama mzazi aliyefahamika kwa jina la Mboka Mwakikagile(20) kuwa Prisca ni shangazi yake Salehe hivyo anakuja kumwona mtoto aliyezaliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa Askari huyo ambapo amesema kuwa ikithibitika kutenda kosa hilo atafikishwa mahakama ya kijeshi na baada ya taratibu hizo kukamilika atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo mkabili.

Mtuhumiwa amekamatwa April 17 mwaka huu huko eneo la Meta Jijini Mbeya majira ya saa nne asubuhi akiwa na mtoto huyo mkononi ambapo alitiwa nguvuni na kufikishwa makao makuu ya Polisi Mkoa Forest ya Zamani kwa mahojiano zaidi.

Msangi amesema kuwa Salehe na Prisca hawana mahusiano ya Damu ila wana mahusiano ya kibiashara ambapo wanaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.

Na Mbeya yetu



No comments: