Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, October 22, 2014

TFDA MBEYA YAADHIMISHA WIKI YA CHAKULA TANZANIA

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Kanda ya Nyanda za juu kusini, Rodney Alananga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya maadhimisho ya wiki ya chakula Tanzania.

Baadhi ya waandishi wa habari

MAMLAKA ya kudhibiti chakulana Dawa Kanda ya Nyanda za juu kusini(TFDA) Mbeya imesema itaadhimisha wiki ya chakula Tanzania kutoa elimu kwa wananchi.

Aidha Mamlaka hiyo pia imewashauri wananchi  kuzingatia usafi kabla na baada ya kula ili kuepukana na magonjwa ya milipuko kwa kunawa mikono kabla ya kula, kuandaa chakula na baada ya kutoka chooni.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Kanda ya Nyanda za juu kusini, Rodney Alananga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya maadhimisho ya wiki ya chakula Tanzania.

Alananga alisema wiki hilo linaadhimishwa kuanzia Oktoba 20 hadi 26, mwaka huu ambapo kitaifa inafanyikia katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke jijini Dar es salaam na kwamba kila Kanda itaadhimisha kwa shughuli mbali mbali zenye lengo la kuhamasisha wananchi kuzingatia usafi kwenye chakula.

Alisema kikanda katika wiki hilo watatumia muda mwingi kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kwenye jamii kuhusu umuhimu na madhara ya kutokujali usafi kwenye chakula, kutoa maonesho mbali mbali ya bidhaa na kugawa vipeperushi vitakavyokuwa vikielimisha wananchi.

Alisema pia watahakikisha wanaleta chachu kwa jamii ili kuleta mabadiliko ya kujenga tabia ya usafi,kukataa kutumia chakula ambacho sio salama, kuzingatia mfumo mzima wa chakula kuanzia uzalishaji hadi kumfikia mlaji kwa kuzingatia kanuni bora za chakula salama.

Alisema chakula salama ni kile ambacho hakina dalili za kuingiliwa na uchafu wa aina yoyote ambao binadamu akitumia anaweza kupata madhara ya muda mrefu au madhara ya papo hapo kutokana na uwepo wa vijidudu, uchafu wa kawaida au kemikali.

Alisema kauli mbiu ya Wiki la chakula ni Chakula salama ni msingi wa afya bora na maendeleo na kufafanua kuwa kauli mbiu hiyo imelenga umuhimu wa kulinda afya kuzalisha na kuleta maendeleo ili kumkwamua kiuchumi mwananchi.

Aliongeza kuwa kama watu hawatazingatia usafi wa chakula wanaweza kupata madhara mbali mbali kama vile magonjwa ya milipuko kama kipindupindu, vifo, matumbo ya kuhara,kukosa soko la chakula kitaifa na kimataifa kutokana na kufungiwa baada ya kuona kinaleta madhara kwa watumiaji.

Alisema ili kuepuka hali hiyo ni vema kila mtu akazingatia usafi wa chakula hususani waandaaji na wamiliki wa mahoteli ili kuhakikisha nyumba zao zinakidhi vigezo vya afya, wahudumu kuzingatia usafi kabla ya kumhudumia mteja kwa kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kutovaa pete na bangili mikononi na kwenye vidole, kupima afya zao kabla ya kuanza kazi na kupima kila baada ya miezi sita.

Mwisho.

Na Mbeya yetu

No comments: