Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 22, 2014

WAKULIMANA MAAFISA KILIMO JIJI LA MBEYA WATEMBELEA SKIMU YA UMWAGILIAJI IGOMELO MBARALIILI KUJIFUNZA.

Mwenyekiti wa Ushirika wa Skimu ya umwagiliaji ya Igomelo iliyoko Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Nelson Vicent akitoa ufafanuzi wa maswali mbali mbali alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa wakulima na Maafisa kilimo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Afisa Umwagiliaji wa Skimu ya Igomelo, Ramadhani Makombe akielezea namna wakulima wanavyonufaika na Skimu hiyo sambamba na utunzaji wa maji.


Afisa Umwagiliaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mwakibete Kasilati akitoa muongozo juu ya lengo la ziara ya wakulima na Maafisa kilimo wa Jiji la Mbeya katika Skimu ya Igomelo.


Afisa Kilimo Jiji la Mbeya, Advera Kahitwa akiwa Sambamba na Afisa umwagiliaji wa Jiji Mwakibete Kasilati ambao waliongoza msafara wa Wakulima 15 na Maafisa kilimo 18 kutembelea Skimu ya Igomelo wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wenyeji wao.


Mjumbe wa bodi ya Skimu ya umwagiliaji ya Igomelo, Zainabu Mgeni akisoma taarifa kwa wakulima na maafisa kilimo kutoka Jiji la Mbeya waliowatembelea.

Baadhi ya Wakulima na maafisa kilimo kutoka Jiji la Mbeya wakifuatilia kwa makini maelezo kutoka kwa wenyeji wao viongozi wa Skimu ya Igomelo.


 Afisa kilimo kutoka Iganjo jijini Mbeya, Elizabeth Mushi akiuliza maswali juu ya changamoto ya soko kwa wakulima wa Skimu ya Umwagiliaji ya Igomelo.

Katibu wa Ushirika wa Skimu ya Igomelo, Japhet Mvukali akifafanua jambo.

Maafisa Kilimo kutoka Jiji la Mbeya wakichukua dondoo mbali mbali zilizobandikwa katika mbao zilizomo kwenye ofisi za ushirika wa skimu ya Igomelo.

Mwekiti wa Skimu ya Igomelo, Nelson Vicent akiwaonesha baadhi ya maelezo yaliyobandikwa kwenye ubao wa matangazo wakulima na maafisa kilimo kutoka jijini Mbeya.


Afisa Umwagiliaji wa Skimu ya Igomelo, Ramadhani Makombe, akitoa maelezo kwa Wakulima na maafisa kilimo kutoka Jijini Mbeya.

Mkulima wa Nyanya katika shamba la Skimu ya Igomelo, Devotha Katawa akitoa maelezo juu ya maendeleo ya mazao katika shamba lake.

wakulima na Maafisa Kilimo kutoka Jiji la Mbeya wakiwa shambani wakijionea namna mazao yanavyostawi kutokana na kilimo cha umwagiliaji.

Afisa Kilimo jiji la Mbeya, Advera Kahitwa akiwaongoza Wakulima na maafisa Kilimo kupata maelezo mbali mbali juu ya kilimo cha umwagiliaji kutoka kwa Mkulima wa Skimu ya Igomelo Devota Katawa.


Wakulima na Maafisa Kilimo kutoka Jiji la Mbeya wakipata maelezo katika shamba la Nyanya.

Baadhi ya mabango yakionesha hatua mbali mbali zinazochukuliwa na uongozi wa Skimu ya Igomelo kwa wakulima wanaokiuka taratibu za uendeshaji wa Skimu.

Wakulima na maafisa kilimo wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya walipata fursa pia ya kutembelea Banio kubwa la Maji katika Mto Mbarali na kupeleka maji katika Skimu ya Igomelo.

Afisa Kilimo Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Advera Kahitwa akiwaonesha wakulima na Maafisa Kilimo jiji la Mbeya namna matunda ya pilipili hoho yalivyo makubwa yaliyovunwa tayari kupelekwa sokoni.

Picha ya Pamoja katika ya Maafisa Kilimo Jiji la Mbeya na Wenyeji wao ambao ni viongozi wa Skimu ya Igomelo.


Picha za pamoja za wakulima kutoka Skimu za Iganjo, Imbega na Ikanga wakiwa wamepiga na Maafisa Kilimo wa Jiji la Mbeya.


picha ya pamoja ya Wakulima na maafisa kilimo Halmashauri ya Jiji la Mbeya pamoja na viongozi wa Skimu ya umwagiliaji ya Igomeli baada ya kukamilisha kwa ziara yao ya kimafunzo.

Mojaya Maghala ya kuhifadhia vitunguu vya Wakulima wa Skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.


Mmoja wa Wakulima wa Vitunguu katika Skimu ya Umwagiliaji ya Igomelo wilayani Mbarali akichukua zao hilo kutoka katika ghala alilokuwa amehifadhia tayari kwa kupeleka sokoni.

WAKULIMA nchini wametakiwa kuwawabunifu katika kuendesha kilimo chenye tija na sio kubweteka majumbaniwakisubiri wataalamu ili waweze kuwapa mbinu ili hali Serikali inakabiliwa naupungufu wa maafisa kilimo.


Wito huo ulitolewa  na Afisa umwagiliaji wa Skimu ya Igomeloiliyopo wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya, Ramadhan Makombe, alipokuwa akitoamaelekezo kwa Wakulima 15 na Maafisa Kilimo 18 kutoka Halmashauri ya Jiji laMbeya waliofanya ziara ya kimafunzo katika Skimu hiyo ambayo ni skimu ya nnekwa ubora kitaifa.


Makombe alisema Mafanikio yaSkimu ya Igomelo yametokana na wakulima kutozubaa kusubiri maafisa Kilimo ilikuwapa maelekezo mbali mbali bali wao wenyewe wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali ili kuongeza uzalishaji katika Skimu zao ambapo hulazimika kuwatafutawataalam pindi wanapokwama


. Alisema Skimu hiyo yenyewakulima 294 wakiwemo wanawake 65 na wanaume 179 katika Shamba lenye ukubwa waHekta 312 ni vigumu kwa wataalam kuweza kuwafikia wote kwa wakati mmoja jamboambalo linaweza kukwamisha uzalishaji wa mazao.


Naye Mwenyekiti wa Ushirika waIgomelo unaosimamia Skimu hiyo, Nelson Vicent, alisema wakulima katika Skimuhiyo wamenufaika na mafunzo mbali mbali wanayoyapata kutoka kwa wataalam jambolililopelekea kila mtu kuwa mtaalam wa kilimo na kujikita katika kilimo chenyetija.


Aliongeza kuwa uwepo wa Skimuhiyo inayotegemea maji kutoka Mto Mbarali hivyo kuwezesha kulima kilimo chaumwagiliaji kwa kipindi chote cha Mwaka imesaidia kupunguza changamoto yaVijana kukimbilia mjini na kuacha shughuli za kilimo vijijini na kufanya kijijicha Igomelo kutokimbiwa na Vijana.


Alisema tangu kuanzakujihusisha na kilimo cha umwagiliaji katika Skimu hiyo mwaka 1998 kumekuwa nautofauti wa uzalishaji wa mazao wanayolima ambapo alisema uzalishaji wa mahindiumeongezeka kutoka Tani 1.5 kwa Hekta hadi tani 3.7, Mpunga kutoka tani 2 haditani 4, Vitunguu kutoka tani 13 hadi tani 26 na Nyanya kutoka tani 5 hadi tani35.


Kwa upande wake kiongozi waMsafara wa Wakulima na Maafisa kilimo kutoka Jiji la Mbeya, Afisa umwagiliajiwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mwakibete Kasilati, alisema lengo la kufanyaziara hiyo ni kutaka Wakulima na maafisa kujifunza namna ya uendeshaji wa skimu unavyofanywa.


Aliyataja malengo mengine kuwani kujua namna ya utunzaji wa skimu hadi kupata mafanikio na kuwa skimu ya nnekwa ubora kitaifa pamoja na namna walivyofanya kuimarisha vikundi katika Skimuya Igomelo.


Kasilati alisema katika Ziarahiyo ilihusisha wawakilishi wa Wakulima kutoka Skimu za Iganjo, Ikanga naImbega zote za jijini Mbeya wapatao 15 na Maafisa kilimo 18 kutoka katika Kata  zaHalmashauri za Jiji la Mbeya ambapo walipata nafasi ya kuwauliza maswali mbalimbali viongozi wa Skimu ya Igomelo pamoja na kutembelea eneo la Skimu.


Naye Afisa Kilimo Jiji laMbeya, Advera Kahitwa alisema pamoja na Jiji la Mbeya kuendelea kukua hivyokuwa na ufinyu wa ardhi ya kuendeshea kilimo bado kuna ulazima wa kutengamaeneo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.


Mwisho. 
Na Mbeya yetu


No comments: