Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, March 26, 2015

HATARI: KILIMO CHA ZAO LA MAHINDI ENEO LA SAE JIJINI MBEYA CHATIA HOFU KWA WAKAZI WA ENEO HILO KUTOKANA NA VITENDO VYA UKABAJI VINAVYOENDELEA. JE JIJI WAMERUHUSU KILIMO HIKI?

Wananchi walalamika kuwa wanataarifa kuwa Jiji walikataza kilimo hiki lakini watu wameendelea kulima

Wakazi wanaokaa Jirani na pembezoni mwa Mahindi hayo waingiwa hofu ya vibaka
Mahindi hayo yawa makazi ya Vibaka, Wavutabangi na waalifu wengine.
Haya ndiyo mahindi ambayo yapo Jirani kabisa na Mitambo ya Tanesco Sae Jijini Mbeya ambapo wakazi wamepata hofu kubwa kutokana na kutokuwa zao lakini Pori
 Ingawa watoto wanapita hapa lakini ni eneo ambalo ni hatari 
 vijana wengi wacheza Kamari , wahuni wengine na wavuta Bangi wanashinda eneo hili la Sae Nyuma ya Mitambo ya Tanesco
 Hapa sio salama
 Hii njia zamani ilikuwa inapitika kwa Urahisi sana kwa sababu kulikuwa hakuna mahindi kabisa lakini sasa wakazi hawapiti kwa sababu ya haya mahindi hata mchana peupe watu hawapiti.
 Bado haya ni matatizo sana eneo hili 
 Vibaka hukimbilia eneo hili
 Makazi ya Vibaka
 

 Je kwa Hali hii wananchi wataishi kwa amani... Huku jiji walikataza lakini iweje  Mahindi haya yalimwe?
 Moja ya Eneo Korofi Sae Jijini Mbeya ambapo watu wengi wamekuwa wakikabwa 
Swali ni Je Jiji wameruhusu Shughuli za Kilimo cha Mahindi eneo la Jiji kama ilivyo Sae Mbeya? Je wananchi kama wanajua hawatakiwi kulima Mahindi haya kwa nini wameendelea kufanya hivyo? Hii ni sinto fahamu ambayo wakazi wa Eneo la Sae pia hawana majibu kwa kuwa wameendelea kupatwa na hofu kubwa kutokana na vitendo vya kuongezeka kwa wakabaji, wavuta Bangi, Wacheza kamali na makazi ya Vibaka. 

Picha na Mbeya yetu

No comments: