Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, April 16, 2015

SAFARI LAGER WEZESHWA YATOA MAFUNZO KWA WAJASILIAMALI MBEYA.


 Mwezeshaji wa mkufunzi kutoka TAPBDS, Sizya Puya akiendesha mafunzo kwa wajasiliamali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika jijini Mbeya.
 Mwezeshaji wa mkufunzi kutoka TAPBDS, Sizya Puya (aliyesimama mbele)akiendesha mafunzo kwa wajasiliamali kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini yaliyofanyika jijini Mbeya
 Wajasiliamali wakiwa katika mafunzo
  Mfanyabiashara wa Hotel ya Mbeya Peak, Lusajo Mwakoba akielezea matarajio yake
 Mfanyabiashara wa Kuchomelea, Stela Mwashalinda akieleza matarajio yake baada ya mafunzo kutoka safari lager wezeshwa
 Mkufunzi wa wajasiliamali akiendelea kutoa mada.
Mwezeshaji akitoa maelekezo kwa washiriki wa mafunzo

WAJASILIAMALI 12 kutoka mikoa ya Kanda ya nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo juu ya kusimamia na kuendesha biashara zao.

Mafunzo hayo yameratibiwa na Kampuni ya bia Tanzania(TBL) kupitia shindano la Safari lager wezeshwa yanayofanyika kwa siku tano katika hoteli ya Peter Safari iliyopo Ilomba jijini Mbeya, mafunzo ambayo yatatolewa kuanzia Aprili 13 hadi Aprili 17, mwaka huu.

Akizungumza katika mafunzo hayo, mkufunzi mwezeshaji wa usimamizi na uendeshaji wa biashara, Sizya Puya kutoka kampuni ya TAPBDS, alisema lengo la mafunzo ni kuwawezesha wafanyabiashara waliondani ya biashara zao kuacha kuendesha kimazoea bila tija.

Alisema Kampuni ya Bia ya TBL imekuwa na mchakato wa kuwainua wajasiliamali wadogo kwa kuwaongezea mitaji katika biashara zao kupitia shindano la Safari lager wezeshwa ambapo mjasiliamali hujaza fomu maalumu kisha huchujwa na kuwapata waliokidhi vigezo na masharti.

Aliongeza kuwa mchakato wa kuwapata wafanyabiashara hao ulianza mwezi Februari mwaka huu ambapo wafanyabiashara waliojitokeza walikuwa 29 ambao walichujwa baada ya kutembelea katika maeneo yao ya biashara na kubakia 12 watakaopatiwa mafunzo kisha vifaa walivyoomba kwa ajili ya biashara zao.

Puya alisema wajasiliamali waliofanikiwa kupita kwenye mchujo wanatarajia kukabidhiwa vifaa vyao mwishoni mwa mwezi huu, vitu ambavyo vimeombwa na mfanyabiashara mwenyewe ili kuongeza nguvu kwenye mtaji wake.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliipongeza kampuni ya bia (TBL) kwa kuanzisha mchakato ambao huwainua wafanyabiashara ambao mara nyingi wanashindwa kuendesha biashara zao kutokana na kukosa mitaji ya kutosha kumudu mahitaji mbali mbali.

Mfanyabiashara Lusajo Mwakoba anayeendesha biashara ya Hoteli inayojulikana kwa jina la Mbeya Peak alisema aliingia kwenye shindano ili aweze kuboresha huduma ya chakula kwa ajili ya wateja wake pamoja na kuanzisha upikaji wa vyakula kwenye masherehe.

Alisema amelazimika kuboresha sehemu ya chakula akiamini kuwa kitakuwa kichocheo cha wateja kufika kupata huduma za vinywaji na malazi ambao anatarajia kuongeza wapishi wazuri pamoja na vitendea kazi.

Naye Stellah Mwashalinda mfanyabiashara wa kuchomelea alisema matarajio yake ni kuongeza vitendea kazi kwani mara nyingi alikuwa akikosa baadhi ya kazi kutokana na ukosefu wa mashine kwani wateja wake wengi wanatoka nje ya eneo lake la kazi.

No comments: