Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, May 18, 2015

BENKI YA NMB MBEYA YATOA MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE YA MSINGI LUBELE WILAYANI KYELA.‏

Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati 60 yenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni tano kwa mkuu wa wilaya ya Kyela, Dkt THEA NTARA kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi LUBELE.

 Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za juu kusini LUCRESIA MAKIRIYE akikabidhi madawati serikali ya wilaya ya kyela akishikana mkono na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela CLEMENCE KASSONGO.


Meneja wa NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini akishikana mkono na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kyela GABRIEL KIPIJA.

KATIKA kuhakikisha uhaba wa Madawati unapungua katika shule za msingi mkoani Mbeya,Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya nyanda za Juu kusini,LUCRESIA MAKIRIE amesema benki hiyo itaendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na serikali katika uboreshaji wa sekta ya elimu nchini.

MAKIRIE ametoa kauli hiyo wakati wa Hafla ya kukabidhi Madawati 60 katika shule ya msingi Lubele yenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni tano,na kuongeza kuwa NMB wataendelea kuchangia na uimarishaji wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari wilayani Kyela.

Alisema Benki hiyo itaendelea kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika kwa kutoa misaada mbali mbali pale inapokuwa inahitajika na kuongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa benki hiyo kurudisha fadhila kwa wateja wake kupitia huduma za kijamii.

kutokana na msaada huo, Utakuwa umepunguza pengo la upungufu wa madawati katika Shule za Wilaya ya Kyela ambayo hadi sasa inakabiliwa na upungufu wa madawati 1600 na kupelekea wanafunzi kusoma kwa shida baada ya kubanana darasani.

Na Mbeya yetu

    No comments: