Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, July 26, 2015

BALAA JIJINI MBEYA MAGARI MATATU YAGONGANA, LIPOBASI LA AL SAEDY.

Mwonekano wa Ajali hiyo

Gari Ndogo ambayo ni IT ikiwa pembeni mara baada ya kungoga Noah kwa nyuma.



Polisi wa Usalama Barabarani wakiwa katika eneo la tukio mara baada ya Ajali hiyo kutokea


Abilia waliokuwa kwenye basi la Al saedy wakiwa na mizigo yao mara baaada ya ajali hiyo kutokea Maeneo ya mama john jijini Mbeya leo asubuhi.


Mwonekano wa Gari ndogo aina ya Noah ambayo imegongwa na Basi la kampuni ya Al saedy ikiwa inavutwa na gari ya Polisi.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo jijini Mbeya baada ya magari matatu kugongana katika eneo la Mama John ambapo magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni basi la Al Saedy linalofanya safari zake kutoka Mbeya kwenda mkoani Dar es Salaam, Noah na gari lingine dogo (IT) Ajali hiyo imetokea wakati dereva ambaye hajafahamika kwa jina mara moja wa basi la Al Saedy lenye namba za usajili T T830 BQG lililokuwa limetokea kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya kuelekea Dar es Salaam alipokuwa akitaka kulipitagari dogo katika eneo hilo ambapo akakutana uso kwa uso na gari dogo aina ya Noah lenye namba za usajili T 969 BWG lililokuwa likitokea Uyole na likiwa na watu watano walionusurika kifo.
 Taarifa za mashuhuda kutoka eneo la tukio zinasema kuwa baada ya Basi hilo la abiria kugongana na Noah gari lingine dogo IT lililokuwa likielekea Tunduma kutoka Dar es Salaam liligonga Noah upande wa nyuma. Kutokana na kilichoshuhudiwa katika eneo la ajali, mashuhuda vwametanabaisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na kutokuwa makini kwa dereva wa basi hilo ambalo abiria wake wote wamenusurika kujeruhiwa.
 Aidha ajali hiyo imesababisha majeraha makubwa kwa dereva wa Noah ambaye amevunjika mguu wake pamoja na dereva wa gari dogo IT ambao wote waliwahishwa hospitalini kupatiwa huduma ya kwanza (wote hawakufahamika majina yao mara moja). Hakuna vifo katika ajali hiyo.

No comments: