Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, February 3, 2016

MIMEA VAMIZI HATARI KATIKA HIFADHI YA MLIMA RUNGWE

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira asilia Mlima Rungwe, Innocent Lupembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na miti aina ya Mipaina iliyovamia hifadhi hiyo na mikakati ya kuiondoa.


Baadhi ya Miti isiyo rafikiwa mazingira na vyanzo vya maji ikiwa imepandwa karibu kabisa na Hifadhi ya Mlima Rungwe ambapo ikikomaa hupeperusha mbegu zake ndani ya Hifadhi na kupelekea kuharibu Ikolojia ya Mlima
 
HIFADHI ya Mlima Rungwe uliopo katika Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya iko hatarini kupoteza uoto wake wa asili kutokana na kuvamiwa kwa miti ya kisasa aina ya mipaina inayopoteza Bainoai za mlima huo.
 
 
Hayo yalibainishwa mwishoni mwa Wiki na Mkurugenzi msaidizi wa Shirika la kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira Kanda ya Mbeya(WCS), Sophy Machaga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoka Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)waliotembelea hifadhi yam lima huo.
 
 
Alisema mlima huo una bainoai pekee zinazowezesha viumbe hai na uoto wa asili kuendelea kustahimili lakini uwepo wa mimea vamizi aina ya mipaina hupoteza sifa kutokana na sifa zake za kuharibu mazingira na kukausha vyanzo vya maji.
 
Machaga alisema a uvamizi wa miti ya kigeni (Pinus patula) iliripotiwa na WCS kwa mara ya kwanza mwaka 2004 ikiwa imevamia hekta 64lakini baada ya hapo imeendelea kuongezeka na kufikia zaidi ya hekta 100 eneo lililovamiwa.

Kwa upande wake Mhifadhi Mazingira asilia Mlima Rungwe(TFS), Innocent Lupembe alisema  tayari kuna mpango wa usimamizi ambao utaanza kutekelezwa mwaka huu 2016.
 
Alisema katika mpango hu0 kuna mpango mdogo wa kuondoa miti vamizi aina ya misindano (Pines) ambayo ni tatizo kubwa katika hifadhi ya Mlima Rungwe kwani inahatarisha ikolojia yake.
 
 
“Katika kutekeleza mpango mdogo wa kuondoa miti vamizi, hatua kadhaa tayari zimefikiwa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha andiko (proposal) makao makuu TFS. Katika mpango huo mdogo tunataraji kufuata hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kupima ujazo wa miti na eneo lililovamiwa kisha kutoa elimu kwa jamii inayozunguka hifadhi juu ya kusudio la kuiondoa miti hiyo. Hii itahusisha pia viongozi mbalimbali katika ngazi za kata na wilaya. Shirika la WCS litasaidia katika kufanikisha zoezi hili. Aidha uondoaji wa miti hii unatarajiwa kufaidisha TFS na jamii inayozunguka hifadhi” alifafanua Mhifadhi huyo.
 
 
Aliongeza kuwa changamoto kubwa katika jamii inayoizunguka hifadhi hiyo ni shule zake kukosa madawati hivyo baada ya kuvunwa miti hiyo walitarajia kutengeneza madawati lakini imegunduliwa kuwa mbao zake ni laini hazifai kwa madawati.
 

No comments: